MWANZA:MKUU WA MKOA WA AZINDUA SHEREHE ZA JUBILEE KANISA LA WAADVENTSTA WA SABATO KIRUMBA
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mh John Mongella, akitoa hotuba katika uzinduzi wa
sherehe za Jubilee ya Miaka 50 jijini Mwanza Katika katisa la
Waadventista Wasabato Kirumba Mwanza Tanzania. terehe 30/06/2016. Kutoka Kutosho, ni Mchungaji Kuyenga ambaye pia ni mkalimani wa Mgeni kutoka Marekani Prof Leal Ceasar, Kutoka kulia ni Mchj Yusufu Lutonja, na Askofu Mkuu wa Jimbo La Nyanza Kusini(South Nyanza Conference mchj Sadock Butoke |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh John Mongella,Juni 30,2016 amezindua Sherehe za Jubilee ya Miaka 50 ya injili jiji la Mwanza katika
kanisa la Waadventista Wasabato Kirumba Mwanza Tanzania.
Mkuu huyo katika hotuba yake, amelipongeza kanisa la Kirumba kuwa na jubilee ya miaka 50 Lakini pia amelipongeza kwa huduma ya malezi ya vijana wa kanisa hilo wakingali wadogo na kwamba kwa kufanya hivo ni kuliandaa kanisa na Taifa kwa ujumla kuwa na viongozi waadilifu.
Mkuu huyo
wa Mkoa pia ameyataka madhehebu ya dini yawe mstari wa mbele katika
kukemea maovu ili Taifa letu lidumu kuwa na Amani aidha amewasihi
waumini kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania.
Miongoni mwa wageni
waalikwa waliohudhuria Hafra hiyo ni, Wachungaji wastaafu wa kanisa la
Waadventista Wasabato, Familia asisi za kanisa la Kirumba
linalosheherekea miak,Mh Diwani wa Kata ya Kirumba Mwanza,
Mh Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Kirumba Bondeni, waumini wa
kanisa,wananchi majirani katika eneo la Kirumba, watu mashuhuri , na
viongozi wa vyama vya siasa,ndugu jamaa na marafiki; Bila kumsahau Prof
na Mchungaji Leal Caesar kutoka Makao Makuu ya kanisa la Waadventista
Wasabato nchini Marekani.
Katika ziara hiyo Mh. Mkuu wa Mkoa
alipata nafasi ya kutembelea mabanda ya maonesho ya kazi za mikono,Ufunuo Publishing House, Banda la historia na kumbukumbu za kanisa
akiongozwa na mwenyeji wake mchungaji Sadoki Butoke Askofu Mkuu wa Jimbo
La Nyanza Kusini( South Nyanza Conference)katika kanisa hilo, Pia
alipata nafasi kuona shughuli za huduma za afya ambazo zimeendelea kwa
siku 5 mfululizo bure.Huduma ya utoaji damu kwa kujitolea ilikuwa
ikiendelea.
Imetaarifiwa kwamba, huduma hizo za afya zimehudumia watu
wapatao 900 hadi mchana wa siku ya juni 30,mwaka huu.
Post a Comment