MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:GARI LILILOZAMA BAHARINI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI LAOPOLEWA



Gari lililosababisha watu wawili kupoteza maisha jana baada ya kuzama katika  bahari ya Hindi  baada ya kuserereka toka katika Kivuko cha Mv Kigamboni jijini Dar es salaam limeopolewa.

Gari hilo aina ya Toyota Hiace lenye nambari za usajili T 271 CRG,lilisababisha kifo cha aliyekuwa dreva aliyefahamika kwa jina la Dani na abiria Nice Mwakalango,Kaka wa Marehemu Nice,Brown Mwakalango akieleza kuwa walikuwa wakitokea Mbeya katika maziko ya kaka yao na walilikuta gari hilo nje ya Kivuko na kuongea na dreva ili awapeleke nyumbani Vijibweni.

Brown ameeleza kuwa kutokuwepo kwa mnyororo ambao huwa unafungwa mbele kuzuia magari ndiyo japo lililosababisha gari hilo kutumbukia baharini.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.