MTANGAZAJI

IRINGA:DTB YACHANGIA PESA KWA AJILI YA KUPANDA MITI

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akipanda miti jana wilayani humo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti. Benki ya Diamond Trust Tanzania imedhamini shughuli hiyo kwa kuchangia sh. milioni tano. Picha kwa hisani ya DTB.

Benki ya Diamond Trust Tanzania, imedhamini shughuli ya upandaji miti katika Wilaya ya Iringa iliyopo mkoani Iringa kwa kuchangia sh. milioni tano. ambapo Wilaya ya Iringa imeanza rasmi kupanda miti katika maeneo yaliyotengwa na uongozi wa wilaya, ikiwa ni utekelezaji wa programu ya kitaifa ya kupanda na kutunza mazingira inayoanza mwezi huu.

Wilaya ya Iringa inategemea kupanda zaidi ya miti 5,000 ya mbao, mapambo, kivuli na matunda. Programu ya kupanda miti na kutunza mazingira ilizinduliwa rasmi na Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof. Jumanne Maghembe, wiki iliyopita.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakati akizindua kampeni ya kupanda miti jana alieleza kuwa, Wilaya ya Iringa imetenga maeneo makubwa ya hifadhi ya misitu na mazingira ili kuhifadhi na kuongeza kiwango cha maji nchini katika tarafa za Mlolo, Ismani, Kalenga, Pawaga na Idodo.

Pia alisisitiza umuhimu wa miti na misitu katika kuhifadhi maji na umuhimu wa maji kwa viumbe hai. Alisema, upandaji miti na utunzaji wake utasaidia kupata hewa nzuri, maji, mvua, kupunguza joto na kupambana na mabiliko ya tabianchi.

Programu hiyo ya kitaifa ni ya aina yake nchini na inashirikisha serikali kuu, wananchi na sekta binafsi. Akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki katika shughuli ya kupanda miti, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Diamond Trust Tanzania, Ndugu Viju Cherian, alisisitiza umuhimu wa programu ya kupanda miti.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.