MTANGAZAJI

PICHA:UTAMBULISHO WA KIPINDI KIPYA CHA TELEVISHENI CHA KISWAHILI WASHINGTON DC

Oktoba 31,Mwaka huu  Swahili Media Network LLC kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC walitambulisha kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili JAMBO TV SHOW kitakachoonekana kwenye kituo cha Televisheni cha DCTV huko Marekani.

Pia, Swahili Media Network inaandaa kipindi cha Radio cha Jambo America, kinachosikia kupitia WJFK ambayo ni radio-dada ya WPGC chini ya shirika la CBS Radios
Ratiba kamili ya vipindi kutoka Swahili Media Network, itakujia hivi karibuni
 
Mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza (katikati) akizungumza na Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi waTanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme na baadhi ya waliohudhuria uzinduzi huo
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme (wa pili kushoto) ambaye pia alimuwakilisha Mhe Balozi Wilson Masilingi, akimsikiliza mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza
Mshereheshaji wa siku hiyo, Grace Ssebo akikaribisha wageni
Wasanii Adele na Frank wakiimba nyimbo za taifa za Marekani na Tanzania, wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo
Mwakilishi wa balozi, ambaye pia ni Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme, akisalimia wageni wakati wa utambulisho
Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme akitambulisha rasmi kipindi hicho
Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska
Mmoja wa washiriki wa Jambo Show Radio inayotayarishwa na Swahili Media Network, Sala Damali
Mwanzilishi wa Jambo Show Steven Mghaza akielezea kipindi hicho kwa wageni waalikwa
Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska akielezea umuhimu wa radio kwa jamii yetu na muelekeo wake
Mwakilishi wa Ubalozi wa Kenya, Joyce Gasugar, akitoa salaam





Mzee Magali akitumbuiza






No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.