MTANGAZAJI

VIDEO:UJUMBE WA WATOTO KWA WAGOMBEA KUHUSU KUWALINDA DHIDI YA VVU




Maendeleo makubwa yamepatikana katika kupunguza kuenea kwa VVU.
Hata hivyo, ambukizo moja katika kila maambukizo kumi mapya huwapata watoto wanaozaliwa japokuwa asilimia 90 ya maambikizi haya yangeweza kuzuilika. Wasichana pia wamo hatarini zaidi kuambukizwa VVU kuliko wavulana. 


Kila ambukizo jipya la kijana aliye chini ya miaka ishirini linadhihirisha kushindwa kuwapatia vijana elimu ya afya ya uzazi, taarifa, stadi na huduma zitakazowawezesha kujilinda. Unyanyapaa na ubaguzi vinaendelea kudhoofisha uwezekano wa wanawake kupata huduma.
Fanya kazi pamoja na washiriki wote katika kupanua huduma na matibabu yatakayoangamiza kabisa maambukizi ya VVU ya mama kwa mtoto ifikapo mwaka 2016. Hakikisha kuwa watoto wote wenye VVU na UKIMWI wanapata matibabu wanayoyahitaji.
Toa ahadi ya kuongeza rasilimali katika kuwakinga vijana, hasa wasichana dhidi ya VVU na UKIMWI kwa kuunga mkono mpango wa kitaifa wa kuzuia VVU.
Saidia katika kuanzisha huduma za afya zinazowalenga vijana na mipango madhubuti ya stadi za maisha ambazo zitawapa taarifa na kuwawezesha, hasa wasichana kupunguza uwezekano wao wa kuambukizwa VVU na UKIMWI.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.