DAR ES SALAAM:TAMASHA LA MTOTO KIKE LAFANA
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai akiwaasa watoto wa kike kuzingatia elimu kwani ndio nguzo ya
msingi katika maisha yao wakati w siku ya Mtoto wa Kike Duniani
iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Tandale jijini Dar. (Picha na
Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
Na Mwandishi wetu
WAKATI
serikali imekiri kwamba pamoja na kuwa na sheria kali za kuzuia ukatili
kwa watoto bado kuna matukio mengi yanayowanyima watoto uhuru na haki
zao msingi,wadau mbalimbali walioshiriki tamasha la mtoto msichana
wamewataka wasichana kutimiza ndoto zao.
Katika
tamasha hilo lililofanyika katika shule ya msingi Tandale, wilaya ya
Kinondoni mkoani Dar es salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa nane
vipaji mbalimbali vya watoto vilioneshwa na watoto nao kutoa kauli zao
za kutaka haki na ustawi wao kwani wao ni taifa la sasa.
Pamoja
na watoto hao kutoa ushuhuda na kuonesha njia ya kusaidiwa, Mkurugenzi
wa watoto kutoka wizara ya maendeleo ya jamii , jinsia na watoto
Margaret Sawe Mussai pamoja na kuwaambia watoto na jamii kutumia simu
119 kuelezea ukatili, ametaka madawati yaliyopo Polisi kutumika vilivyo
kukabiliana na vitendo hivyo.
Alisema
taarifa zilizopo watoto wa kike asilimia 29 na wavulana asilimia 13
wamenyanyaswa kijinsia wakati wasichana asilimia 14 na wavulana asilimia
6 wamekabiliwa na tatizo la kujaribiwa kuvurugwa kijinsia.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem akizungumza jambo kwenye siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Tandale jijini Dar.
Msaidizi
wa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum akisoma
risala kwenye siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyofanyika katika viwanja
vya shule ya msingi Tandale jijini Dar.
Angel
Benedicto ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani akieleza alipotokea
mpaka kufika alipo sasa wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike
yaliyofanyika siku ya Jumamosi.
Katika
tamasha hilo wasichana wawili walitoa ushuhuda, Binti mdogo Eva Tolage
ambaye alimwandikia barua Rais Barak Obama akihoji Marekani na yeye
binafsi rais Obama na viongozi wa dunia watafanya nini kumsaidia mtoto
wa kike anayekabiliwa na changamoto nyingi hasa wale wa vijijini.
Eva
alimwambia Barack Obama kwamba anataka kutimiza ndoto yake ya kuwa
askari kusaidia jamii, lakini atafikiaje ndoto hiyo wakati kuna
changamoto ya umeme na huku baba yake kazi anazofanya hazimpi kipato cha
kutosha.
Msichana
huyo ambaye aliandika barua kwa ujasiri mkubwa akihoji maendeleo
endelevu yasiyompita binti mdogo alijibiwa na Rais Obama na kutajwa
katika hotuba yake kwenye Umoja wa Mataifa kwamba viongozi wa dunia
akiwemo Barack Obama mwenyewe wamemsikia na watahakikisha tatizo la
wasichana wa Afrika na kwingine kokote linaondolewa na na wanapata
nafasi ya kushiriki katika maendeleo.
Eva
Tolage aliyeandika barua kwa rais Barack Obama wa Marekani na barua
yake kusomwa katika mkutano wa viongozi wa dunia makao makuu ya Umoja wa
Mataifa alitumia mkutano huo kusoma machache aliyoandika. Katika barua
hiyo, Eva mwenye umri wa miaka 15, alielezea jinsi ambavyo bado
mazingira mtoto ni mabovu na hatarishi kiasi cha kumfanya ashindwe
kupata elimu bora, pia kuwa katika hatari ya kukumbwa na vitendo vya
kikatili ikiwa ni pamoja na ubakaji.
Aidha
binti mwingine Angela Benedicto ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Wote sawa alisimulia matatizo ya wasichana wa kazi,adha zao
kutoka kwa wanaume na watoto wa kiume wanakofanyia kazi.
Alisema kwamba mateso wanayoyapata wasichana wa kazi yanastahili kukoma na kwamba ipo haja ya kuwekwa kwa mfumo unawalinda.
Alisema
serikali ina wajibu wa kuwatetea wasichana kupata haki zao, sio tu
kusema shule bure, lakini pia kujenga kujiamini kwa wasichana katika
kutimiza ndoto zao.
Alisema
sababu za kuwepo kwa wasichana wengi wakazi za ndani ni dhuluma
inayoambatana na umaskini katika familia na tamaduni zinazomweka nyuma
mtoto wa kike kiasi cha kulazimika kutafuta kazi za ndani ambazo waajiri
wanakuwa hawana staha.
Katika
tamasha hilo kulikuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo za kuangalia hali
ya afya ya uzazi, elimu ya afya ya uzazi, kupimwa maambukizi ya UKIMWI
na kukaguliwa kwa saratani ya matiti na kizazi pamoja na elimu yake.
Pia kulikuwa na michezo ya kuigiza na sarakasi na mwanamuziki wa kike mwasiti alichombeza kwa nyimbo zake za uadilifu.
Siku ya Mssichana duniani huadhimkishwa Oktoba 11 lakini kwa Tanzania iliadhimishwa Oktoba 10.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai (wa kwanza kulia) akivuta kamba pamoja na wanafunzi wa kike huku
Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi.
Hashina Begum (wa kwanza kushoto) akiungana na timu ya wanaume ambapo
timu ya wasichana iliibuka kidedea.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya nchini Mwasiti akitoa burudani wakati wa
maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika katika viwanja vya
shule ya msingi Tandale.
Vijana wa Temeke wakiendelea kutoa burudani.
Wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali wakipatiwa elimu ya afya na uzazi katika mabanda yaliyopo kwenye maadhimisho hayo.
Elimu mbalimbali zikitolewa uwanjani hapo.
Burudani ya nyimbo kutoka kwa wanafunzi.
.
Mmoja wa wanafunzi akijibu swali.
Picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandale.
Mgeni
rasmi na Mwakilishi wa Shirika la UNFPA pamoja na wadau wanaotetea
masuala ya haki ya mtoto wa kike kwenye picha ya pamoja katika bango
maalum.
Wasanii wakifikisha ujumbe kwa njia ya maigizo.
Wanafunzi wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye siku ya mtoto wa kike duniani.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai (kushoto) na Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu
duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem ( wa pili kushoto) katika picha ya
pamoja na watoa huduma katika mabanda yaliyokuwepo kwenye maadhimisho
hayo.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem
wakisaini vitabu vya wageni kwenye banda mojawapo walilotembelea.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Kike Duniani Mkurugenzi wa
watoto kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Margaret Sawe
Mussai (wa pili kutoka kulia) akipata maelezo kutoka kwa wasichana
wajasiriamali alipokuwa anatembelea mabanda.
Burudani nayo haikuwa mbali katika kusherehesha siku ya mtoto wa kike duniani.
Post a Comment