MTANGAZAJI

THALASSAEMIA– UGONJWA WA DAMU HATARI UNAOWEZA KURITHIWA


Ibrahim (jina limebadilishwa) alizaliwa nchini Tanzania na alipokuwa na umri wa miezi 9 tu alionekana anang’aa na hakuwa na uwezo wa kula na kukua vizuri kama watoto wengine wa umri wake. Alikuwa na maambukizi ya mara kwa mara na vipimo vya damu vilionyesha upungufu mkubwa wa damu na kiwango cha ukosefu wa damu kwa gm 3.5! Ibrahim alikuwa akiishi na chini ya robo ya kiwango cha oksijeni kinachohitajika kwenye damu na alihitaji haraka kuongezewa damu ili kuokoa maisha yake. Vipimo vya damu yake na ya wazazi wake vilithibitisha kuwa alikuwa na thalasemia kuu.

Thalassaemia kuu ni hali ya kurithi ambapo huwa na ukosefu wa chembe nyekundu za damu. Katika mwili seli shina Uboho huzalisha aina tatu za seli za damu katika mwili- nyekundu, nyeupe na chembe chembe za damu. Thalasemia ni hali ya kurithi inayoathiri seli nyekundu za damu. Hutokea wakati mtu anashindwa kuzalisha kiasi cha damu kinachotakiwa. Mwili wako hautafanya kazi vizuri kama chembechembe nyekundu za damu hazizalishi damu ya kutosha yenye afya.

Dkt. Revathi Raj wa  Hospitali za Apollo Chennai anaeleza zaidi kwamba thalasemia ni ya kurithi. Ni kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto kwa njia ya jeni. Watu ambao hurithi jeni za damu mbaya kutoka kwa mzazi mmoja lakini jeni za kawaida kwa mzazi mwingine wanaitwa kitaalamu ‘career’. ‘Carriers’ mara nyingi hawana dalili za ugonjwa mwingine zaidi ya kuoneshwa upungufu mkubwa wa damu. Hata hivyo, wanaweza kurithisha jeni mbaya kwa watoto wao. Watu ambao wana wastani wa kati wa thalasemia wamerithi jeni mbaya kutoka kwa wazazi wote wawili. Kama ‘carriers’ wawili wakizaa mtoto, kuna 25% ya nafasi ya kuwa na mtoto aliyethirika.
Kwa mujibu wa Dkt Revathi Raj madhara ya kuacha thalassaemia bila kutibiwa ni pamoja na kushindwa kwa wengu, ini na moyo. Pia, inaweza kusababisha mifupa myembamba na migumu na mikunjo usoni. Ni kawaida kwamba watoto wasiotibiwa hudumaa ukuaji wa mwili na akili. Watoto wenye Thalasemia huwa wanakufa kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi na maambukizi ikiwa hali hiyo haitatibiwa.
Matibabu pamoja na kuongezewa damu mara kwa mara na dawa za kuzuia maambukizi huweza kupunguza kasi ya ugonjwa. Watoto wenye thalasemia wanaweza kutibiwa kwa kuongezewa damu mara kwa mara. Zoezi hili linatakiwa kufanyika kila baada ya wiki 3 au 4 na husaidia kuweka kiwango cha damu kawaida. Wakati viwango vya damu vikiwa kawaida mtu anaweza kujaribu kuzuia baadhi ya matatizo ya ugonjwa kwa hiyo kuzuia moyo kushindwa kufanya kazi na ulemavu wa mfupa na hivyo kupelekea ukuaji mzuri na afya kwa ujumla.
Hali ya Ibrahim ina maana kwamba wazazi wake walihitaji kusafiri pamoja naye kwa zaidi ya km 1,000 kila mwezi kwa ajili ya kuongezewa damu kutokana na ukosefu wa vifaa vya kutosha Tanzania. Huku kuongezwa damu kulihitajika ili kuendelea kwa maisha yote ya Ibrahim hii ikiwa ni hali ya kudumu.

Wangewezaje kutoa damu kila mwezi? Kwa nini hakuna mtu aliyegundua kwamba walibeba jeni mbovu ambazo zinaweza kuleta madhara kwa mtoto wao? Haya ni baadhi tu ya maswali kadhaa ambayo wazazi wa mtoto huyu wanakabiliwa nayo.

Changamoto nyingine iliyowakumba wazazi Ibrahim ililikuwa kwamba pamoja na kila kuongezewa damu kuna hatari ya madini chuma katika kila kiasi cha damu kinachoongezwa. Kujijenga kwa madini chuma husababisha uharibifu wa moyo na ini na viungo vingine. Kuepuka, kuzuia au kuchelewesha madini chuma kujijenga mtu anahitaji tiba ya madawa kila siku. Kwa bahati mbaya hata hivyo, kwa Tanzania tiba hii si rahisi hivyo kupatikana. 

Maisha kwa Ibrahim yalionekana hatarini sana mpaka baada ya familia kusikia kuhusu BMT kusaidia kumtibu mtoto wao mdogo na kusafiri hadi Hospitali ya Apollo, Chennai nchini India ambako walikutana na Dkt Revathi Raj. Hospitali ya Apollo, India ni jina la kuaminiwa katika BMT kwa ajili ya wagonjwa wa kimataifa, kama hospitali ina si tu yenye timu ya BMT inayosifika, lakini pia masharti magumu sana kudhibiti maambukizi ambayo ni muhimu kwa ajili ya wagonjwa wa BMT.
Kwa BMT ‘Haematopoietic’ seli shina inapatikana kutoka kwa ndugu ambaye hajaathirika anayeendana au mfadhili yeyote na kupandikizwa kwa mtu mwenye thalasemia. Kwa bahati mbaya, Ibrahim hakuwa akiendana na wafadhili wa familia. Hata hivyo, mfadhili waliyeendana kikamilifu katika shina kiini la uboho aliyejisajili nchini India aitwaye DATRI alitoa mwanga mpya wa matumaini.
Mkakati wa kupandikiza uboho kwa watoto katika Hospitali ya Apollo nchini India ina timu ya wataalam wenye ujuzi wa juu na mratibu wa BMT anayefanya kazi kama sehemu ya timu ya wataalam mbalimbali kutoa huduma iliyoboreshwa kwa ajili ya watoto ambao wanapata tiba ya shina. Hospitali za Apollo nchini India zina uzoefu mkubwa nchini humo katika kuhudumia watoto wachanga na wadogo wanaoendelea na upandikizaji wa seli za shina.

BMT ni tiba yenye hatari kubwa ambayo inawezekana kwa asilimia ndogo sana ya wagonjwa iwapo mfadhili uboho anayefaa yupo. Hata kama kiwango cha mafanikio ya BMT ni sawa na 95%, ni kazi ya hatari na huweza kusababisha kifo. Kiwango cha mafanikio hutegemea zaidi iwapo au hakuna uharibifu mkubwa uliofanyika kwa kiungo chochote kama vile madini chuma kwenda mahali pasipofaa.

Dawa mpya katika soko na muendelezo wa ugunduzi katika taaluma ya utabibu imewezesha mchakato wa upandikizaji kuwa salama zaidi, hata kwa watoto wachanga na watoto wadogo. Hospitali Maalum ya Apollo, imelifanya upandikizaji wa seli shina kwa zaidi ya wagonjwa 800 ikiwa zaidi ya robo kati yao waliokuwa na thalasemia na zaidi ya kufanikiwa kwa Zaidi ya 90%.

Ujumbe muhimu zaidi mtu anahitajika kuchukua katika hili ni umuhimu wa kupima wajawazito. Vipimo vya damu vinaweza kuonyesha kama mtu ana thalasemia au ni ‘carrier’ kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba. Dkt Revathi Raj katika Hospitali ya Apollo Chennai anashauri kuwa ni bora kumweleza daktari wako kumpima mtoto wako kiwango cha ‘ferritin’ cha mtoto wako kama ana upungufu wa damu kabla ya maagizo ya vitamini yoyote. 

Ni jambo la kawaida kwa madaktari kutoa maelekezo ya vitamini kwa watoto ambazo huonyesha dalili za upungufu wa madini chuma. Hata hivyo, ni muhimu kuchunguza tahadhari, kwa maagizo ya kuongeza madini chuma kwa ajili ya upungufu wa madini hayo anemia inaweza kuwa sahihi, inaweza kusababisha kuzidi kwa madini chuma kwa watoto wenye aina yoyote ya thalasemia. Jaribio rahisi kuamua kiwango cha madini chuma, au kiwango cha ‘ferritin’, katika mwili wa mtu linaweza kufanywa. Kama mtu anaonekana kuwa na upungufu wa madini chuma, lakini kiwango cha ‘ferritin’ kipo kawaida, pengine wana aina ya kwanza ya ‘beta thalasemia’.

Ndugu kuoana mara kwa mara pia husababisha mtu kuwa ‘carrier’ wa thalasemia. Ndoa kati ya ndugu ziepukwe kwa kuwa kuna ongezeko la ugonjwa wa kurithi na kama inaepukika uchunguzi wa damu kwa wanandoa kabla ya ndoa unashauriwa.

Tunahitaji pia kuongeza uelewa miongoni mwetu Watanzania juu ya umuhimu wa kujitolea kwa kuchangia damu na seli za shina kama msaada kuokoa maisha haya. Kuna matumaini kwa watoto wote kupata nafasi ya tiba kwa kuwa kuna wengi waliojisajili – hasa watu wazima ili kusaidia wagonjwa wote wa thalasemia kuu.


Imechangiwa na:

Dkt. Revathi Raj
Mtaalamu wa magonjwa ya watoto ‘Hematology’, Kupandikiza uboho (BMT)
Apollo Hospitals Chennai

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.