MTANGAZAJI

UBORESHAJI WA USALAMA BARABARANI KWA USAFIRISHAJI WA MASAFA MAREFU

 Fuso ikipita Njiani kwenye Maonyesho ya "NDIO Fuso ni Faida" jijini Dar, Maonyesho hayo yanatarijiwa kupita kwenye Mikoa kama Tanga – Moshi- Arusha- Mwanza –Shinyanga -Kahama- Dodoma – Iringa – Mbeya  na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika
 Wadau wa Usafirashaji wakiwa katika Maonyesho ya 'Fuso ni faida' jijini Dar
 Wadau wakipata maelekezo ya Huduma ya 'Ndiyo Fuso ni Faida'

Na Mwandishi Wetu,
Mtandao wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania inayokadiriwa kuwa na kilometa za mraba 91,049 ambayo ni mara 30 zaidi ya mtandao wa reli ambayo inaambaa kwenye eneo lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 3,682 ikidhihirisha kuwa barabara ndiyo njia kuu inayopendelewa kutumika katika usafirishaji wa mizigo. 
Usafirishaji nchini Tanzania unajumuisha mitandao ya barabara, anga, reli na maji ambapo katika njia zote hizi, barabara na reli zinaongoza zikifuatiwa na maji na anga.  Hakika katika suala la umbali, mtandao wa barabara za Tanzania unashika nafasi ya 51 duniani, kutokana na taarifa zilizonukuliwa katika kitabu “ CIA world fact book”.
Wakati ajali za barabarani zikiendelea kugharimu maisha ya watu, ufanisi wa njia hii ya usafirishaji kwa ujumla wake unahitaji kudumisha ubora wa usafirishaji wa barabara nchini Tanzania kutokana na ufanisi wake, kuokoa muda na kuaminika pamoja na kuchukuliwa kuwa kiunganishi kikubwa cha barabara ndogo kwenye barabara kuu za nchi.

Diamond Motors limited hivi karibuni wamekuwa katika safari ya kuzunguka mtandao huu wa barabara wakihamasisha pamoja na mambo mengine usalama barabarani katika kampeni yao ya “Ndio! Fuso ni Faida” Kampeni hiyo iliyozinduliwa mwezi julai mwaka huu jijini Dar es salaam ilifika katika mikoa ya Tanga-Moshi- Arusha – Mwanza – Shinyanga – Kahama – Dodoma – Iringa – Mbeya – na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika. Pamoja na mambo mengine, kampeni hiyo ilidhamiria kujenga uelewa kwa wateja wake juu ya jinsi ya kuboresha usafirishaji salama wa mizigo kwa kutumia magari ya kisasa zaidi.

Kampeni hiyo pia  ilifika katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo imeunganishwa katika ukanda wa kaskazini na barabara za nchi za jirani kama Kenya na Uganda kupitia mipaka yake ya Namanga ikiwa na biashara nyingi baina ya nchi hizo zinazopitia njia ya barabara. 

 Wakazi na wafanyabiashara waliohudhulia kampeni hiyo walipata fursa ya kujionea sifa zipatikanazo katika malori hayo ya Fuso Fz kutoka Diamond Motors Limted ambayo yanauwezo wa kubeba mizigo mikubwa katika mazingira magumu katika ukanda huo.  “Ni kwa teknolojia ya kisasa ya magari haya mabapo wafanya biashara wanaweza kupata Faida ya biashaza zao kwa kutumia malori haya inayotumia mafuta vizuri, ambapo gari hii ina kifaa maalumu cha kuzuia mafuta yasitumike endapo gari hii inatembea katika mteremko ili kukupa umbali mrefu zaidi kwa mafuta kidogo. 
Mikoa ya Mwanza na Shinyanga ambayo ni kitovu cha biashara, usafirishaji, ushirikano wa kikanda na maendeleo ya kiuchumi katika kanda ya ziwa ikiunganishwa na bandari kavu ya Isaka, ilifikiwa na maonyesho haya ya Fuso Fz.  Mikoa hii pia inaunganisha nchi jirani za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi and Demokrasia ya Kongo ambazo ni nchi zenye biashara nyingi kubwa miongoni mwake na Tanzania.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.