MTANGAZAJI

KIGOMA:MAOFISA WA UNION KONFERENSI YA KASKAZINI MWA TANZANIA YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO WAWASILI KIGOMA KWA AJILI YA MKUTANO MKUU WA KANISA HILO




 
 
 

Maofisa wa Union Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato (NTUC) wamewasili mjini Kigoma kwa ajili ya mkutano mkuu wa Konferensi ya Magharibi mwa Tanzania (WTC) utakaoanza Septemba 28,mwaka huu kwa ajili ya kupanga mikakati ya kazi na uchaguzi wa viongozi watakaoongoza eneo hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

 Maofisa hao ni Mwenyekiti Dr Godwin Lekundayo,Katibu Mch Daudi Makoye na Mhazini Ndugu Matiko ambao walipokelewa na viongozi wa Konferensi hiyo wanaomaliza muhula wao wa uongozi.

Kwa mujibu wa Takwimu za Kanisa la Waadventista Wa Sabato za Mwaka 2014 eneo la Konferensi hiyo ambayo imepanda hadhi ya kuwa konferensi mwaka 2014 lilitambuliwa rasmi  kuwa field mwaka 1990 ambapo kwa idadi ya waumini wa kanisa hilo ni 52,136 miongoni mwa wakazi wapatao 8,985,512 huku kukiwa na makanisa 342.

Mikoa inayojumuisha eneo la Konferensi hii ambayo ni miongoni mwa Konferensi nne za Union Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania ni  Kagera, Katavi, Kigoma, Singida na  Tabora.

Mkutano mkuu wa uchaguzi wa Konferensi hii unatarajiwa kumalizika Septemba 29,mwaka huu na ndio utakuwa unakamilisha mikutano mikuu ya Konferensi nne za NTUC kwa mwaka huu.

Konferensi zingine ni ile ya Nyanza Kusini (SNC),Konferensi ya Mara (MC) na  Konferensi ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania (NETC)

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.