MTANGAZAJI

SHINYANGA:MKUTANO MKUU KONFERENSI NYANZA KUSINI (SNC) WAANZA LEO SEPTEMBA 16,2015

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Konferensi ya Nyanza Kusini ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato wakiwa na kadi za kupigia kura
Maofisa wa Konferensi ya Nyanza Kusini wanaomaliza muda wao kutoka kulia ni Katibu Mkuu Mch Philip Ndikumwami na Mwenyekiti Mch Joseph Bulengela wakitoa maelekezo kwenye mkutano huo leo jioni
Mkutano Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato wa Konferensi ya Nyanza Kusini (SNC) umeanza leo Septemba 16 katika kanisa la Lubaga,Shinyanga.

Eneo hilo ambalo linaonekana kuanzishwa mwaka  1912 na kuwa miongoni mwa maeneo kongwe ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania ambapo takwimu za mwaka 2014 zinaonesha kuwa kulikuwa na makanisa 681,waumini 103,386 katika eneo hilo lenye wakaazi 8,928,461.

Konferensi hiyo inajumuisha waumini wa kanisa hilo toka Mwanza (ukiondoa kisiwa cha  Ukerewe) ,Shinyanga, Geita na Simiyu.

Miongoni mwa matukio yanayotarajiwa kufanyika kwenye mkutano huo unaotarajiwa kumalizika Septemba 18 mwaka huu ni uchaguzi wa viongozi wapya watakaoiongoza konferensi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo,huku Mchungaji aliyekuwa akisimamia idara ya mawasiliano ya konferensi hiyo Mch Aston Mmamba akiwa ameshachaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Huduma Binafsi,Shule Sabato na AMR wa Konferensi ya Kaskazini Mashariki wa Tanzania (NETC).

Taarifa zingine zinaeleza kuwa huenda Mwenyekiti wa SNC aliyepo sasa Mch Joseph Bulengela akastaafu hivi karibuni.
 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.