DAR ES SALAAM:MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI TANZANIA YAELEZA HALI YA MVUA OKTOBA MPAKA DESEMBA 2015
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzani Agness Kijazi |
Mamlaka ya hali
ya hewa nchini Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya tathimini ya mvua za masika na mvua za vuli
kwa muda kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2015.
Mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa Dkt
Agnes kijazi amesema Msimu wa mvua wa miezi ya Oktoba hadi Disemba (vuli)
ni mahususi katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha na Manyara), pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga,
Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba), kanda
ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga) na
kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
Mvua za Oktoba-Novemba-Disemba 2015,
zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani na wastani katika maeneo mengi yanayopata
misimu miwili ya mvua.
Maeneo machache ya kusini mwa nchi yanatarajiwa kupata
mvua za chini ya wastani.
Msikilize Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya hali ya
hewa Agnes Kijazi anaeleza hapa
Post a Comment