MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:TWAWEZA YAELEZA VIGEZO WANAVYOVITAZAMA WATANZANIA KUMCHAGUA RAIS MWAKA 2015

Mkurugenzi wa Twaweza Tanzania Aidan Eyakuze
Asilimia 46 ya wananchi wameripoti kuwa sera, uadilifu na maadili mema  ndio kigezo muhimu watakachokitumia kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Rais,Ubunge na Madiwani October 25 mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Twaweza ya nchini Tanzania Aidan Eyakuze  amesema leo kuwa watanzania wana imani na  tume ya uchaguzi nchini humo
 
Taarifa ya Eyakuze inaeleza kuwa  baadhi ya watanzania wanadhani yule mwenye sera bora atamshinda yule mwenye pesa nyingi kama anavyoeleza hapa



Mkurugenzi huyo anaeleza kuwa  asilimia 76 ya wananchi  wanaamini vyombo vya habari vitaripoti kwa usahihi maswala ya uchaguzi mkuu na asilimia 24 wanasema vyombo ya habari vitakuwa na upendeleo kwa motisha ya fedha.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.