MWANZA:ZAIDI YA WALIMU 2,000 WA MKOA WA MWANZA WANAIDAI SERIKALI YA TANZANIA
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Gratian Mkoba |
Walimu zaidi ya 2,000 mkoani Mwanza wanaidai serikali ya Tanzania
malimbikizo ya mishahara pamoja na gharama za upandishwaji madaraja.
Akizungumza na
waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) mkoani Mwanza, Sibora
Kisheri, amesema wanaungana na Rais wa chama hicho taifa, Gratian Mkoba kuitaka
serikali kuwalipa madeni yao kabla ya Septemba mwaka huu.
Kisheri amesema kuwa baadhi ya walimu wanaidai serikali fedha
za likizo na matibabu na wengine wakisubiri kupandishwa madaraja na kuongeza
kuwa wanaunga mkono kauli ya Mkoba ya kuitaka serikali kulipwa madeni yao kabla
ya Septemba mwaka huu pamoja na kwamba Rais Jakaya Kikwete alishaahidi kuwalipa
wakati mkutano mkuu wa CWT uliofanyika mkoani Arusha.
Naye Katibu wa CWT Mkoa wa Mwanza, Said Mselem, ameiomba serikali wakati wa kupanga bajeti, walimu wawe
wanahusishwa ili inapopitishwa waelewe kilichopitishwa.
Mselem amesema CWT mkoa wa Mwanza hawatakubali kuona mwalimu
yeyote mkoani humo anahamishwa na kupelekwa eneo jingine bila kulipwa gharama
za uhamisho.
Post a Comment