DAR ES SALAAM:UN YAFANYA USAFI SOKO LA TEMEKE STEREO KUADHIMISHA MIAKA 70
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza machache
kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema
(katikati) kabla ya kuanza zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kushoto
ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.(Picha zote na
Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Na Mwandishi wetu
KATIKA
kuadhimisho miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN)
wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa walijumuika na wakazi wa
Temeke katika kufanya usafi kwenye soko la Temeke Stereo.
Shughuli
hiyo wameifanya baada ya wiki iliyopita kufanya shughuli za upandaji
miti katika miteremko ya mlima Kilimanjaro. Wakiwa katika miteremko ya
milima Kilimanjaro walipanda miti 2,000.
Shughuli
hizo za kufanya usafi ambazo ziliongozwa na Mratibu wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, zilifanyika katika juhudi za
kuleta uhalisia wa utunzaji wa mazingira kama umoja huo unavyofanya.
Akizungumza
katika shughuli hizo Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, ambaye
alimwakilisha Mkuu wa Mkoa aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa kusherehekea
miaka 70.
“Nachukua
nafasi hii kupongeza watu wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa
kufanya shughuli mbalimbali kuelekea maadhimisho ya miaka 70 kwa kupanda
miti 2,070 kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro na hili tendo la leo
la usafi kama mwendelezo wa kaulimbiu inayohimiza utunzaji wa mazingira
ya“ Sayari moja, watu bilioni 7: Ulinzi wa mazingira ni wajibu wetu,”
alisema.
Akisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na usafi, Mkuu huyo wa wilaya alisema wajibu wa kutunza mazingira ni wa kila mtu.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa
Mataifa katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ikiwemo
kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa wananchi na wafanyabiashara
wa soko la Temeke Stereo mwishoni mwa juma. Kushoto ni Kaimu Mwakilishi
Mkazi wa FAO nchini, Patric Otto. Wa tatu kulia ni mgeni rasmi Mkuu wa
Wilaya Temeke, Sophia Mjema, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Celestine Mushy (wa pili kulia) na Mkuu wa Idara ya Usafi na
Mazingira manispaa ya Temeke, Ally Hatibu.
“Kutunza
mazingira si wajibu wa mtu mmoja. Ni wajibu wako kama ilivyo kwa jirani
yako. Kunapokuwepo na watu wengi mara nyingi hutokea watu ambao
hawajali wala kuona umuhimu wa kutunza mazingira, umuhimu wa kufanya
haya.
“
Nawaomba wote mlioshiriki katika shughuli hii leo kuwa watu wa kuchunga
mazingira katika maeneo yenu mnayofanyia kazi na majumbani
kwenu.Hakikisheni mnafundishana na majirani zako katika suala hili na
kuhakikisha kwamba kila mmoja anayekuzunguka anawajibika katika kutunza
mazingira.”
Akisisitiza
menejimenti ya mazingira, Rodriguez, alizungumza kwamba mabadiliko ya
tabia nchi na mazingira endelevu ndio ajenda kuu katika malengo endelevu
ya maendeleo (SDG’s).
“Mwaka huu jumuiya ya kimataifa itakubaliana kuhusu SDGs na
kukamilishwa kwa malengo ya milenia (MDGs). Malengo ya milenia
yamewezesha kupatikana kwa mabadiliko makubwa katika kukabiliana na
umaskini, afya bora na kiwango kikubwa cha watu wanaojiunga na shule.
Mataifa ya Umoja wa Mataifa kwa kupendezwa na mafanikio ya MDGs sasa
wanataka kukubaliana kuhusu SDGs.
“
SDG itakuwa na vipengele 17 kikiwamo cha mabadiliko ya tabia nchi.
Umoja wa Mataifa umechagua suala la mabadiliko ya tabia nchi kuwa ndio
kipaumbele cha mwanzo kwani imebaini kwamba ni tishio kwa maendeleo
endelevu.
Hii inatokana na ukweli kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli na ni vyema kila mtu kuwajibika ili kuhakikisha mazingira yetu yanaendelea kuwa mazuri-tukianzia na mazingira yetu yanayotuzunguka” alisisitiza.
Hii inatokana na ukweli kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli na ni vyema kila mtu kuwajibika ili kuhakikisha mazingira yetu yanaendelea kuwa mazuri-tukianzia na mazingira yetu yanayotuzunguka” alisisitiza.
Rodriguez
alizitaka jamii mbalimbali kutoa kiipaumbele katika kusafisha mazingira
na usafi binafsi hasa kipindi hiki ambapo kumezuka ugonjwa wa
Kipindupindu kwa mikoa ya Dar es salaam na Morogoro.
“Usafi wa soko hili ni muhimu kwa ajili ya afya yako na uhai mrefu.
Afya njema inatuwezesha kuendelea kufanya shughuli zetu mbalimbali za
kuchangia ukuaji wa uchumi.Hebu angalia pembeni mwako imetuchukua saa
chache kusafisha soko la Temeke na je hamuoni tofauti? Nawaomba wakazi
wa Temeke na wafanyakazi wa soko hili kufanya shughuli hizi kila siku
kwani maisha yao, afya yao na uchumi unategemea soko hili.”
Pia
aliwaalika wananchi wote katika sherehe za miaka 70 za Umoja wa
Mataifa zitakazofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Oktoba 13 ili kushiriki
kikamilifu katika kuadhimisha siku hiyo ya Umoja wa Mataifa.
Pia alihimiza serikali kuendelea kuelimisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Wilaya Temeke, Sophia Mjema akitoa nasaha zake kwa
wananchi na wafanyabiashara wa soko la Temeke Stereo, ambapo aliwataka
kuzingatia usafi wa maeneo yao ya biashara pamoja na majumbani ili
kuepeukana na mlipuko wa Kipundupindu.
Katika
hafla hiyo ya kusafisha soko la Temeke, Umoja wa Mataifa na serikali ya
Tanzania kwa pamoja walitoa vifaa vya kufanyia usafi vyenye thamani ya
shilingi milioni 10. Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa menejimenti ya soko
la Temeke.
Watu
wengine walioshiriki katika shughuli hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy; mkuu wa wilaya ya
Temeke Mheshimiwa Sophia Mjema, akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam na maofisa wengine wa serikali na wakazi wa Temeke.
Balozi
Mushy katika risala yake ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya usafi
aliitaka jamii kutambua kwamba usafi ni jukumu la kila mmoja wetu kwani
bila usafi madhara yake ni makubwa ikiwamo ya kutunzwa kwa mazingira.
Alilitaka
jiji la Dare s salaam ambalo linalinganishwa na majiji mengine duniani
kama Nairobi, Kenya; Pretoria Afrika Kusini, Washinton DC na Paris
kujifunza kuwa wasafi kwani hata mlipuko wa sasa wa Kipindupindu ni
dalili tosha ya kukosekana kwa usafi.
Aidha
alisema kwamba suala la usafi si lazima kwenda kujifunza nje kwani ipo
miji na mikoa misafi ambayo inaweza kuulizwa wamefanikishaje jambo hilo.
Aliitaja miji hiyo ni Moshi, Iringa na Mwanza.
Alisema
katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, wameamua kufanya usafi
wa mazingira katika soko la Temeke kuonesha kwamba inawezekana kufanya
usafi kwa kuwajibika kwa lengo la kufanya mazingira yawe masafi na ya
uhakika.
Kwa kutekeleza usafi kwa maana nyingine kutasaidia kuondoa gharama zinazoambatana na uchafu wa mazingira.
Alitaka kila mmoja katika soko hilo kuanzia wakulima hadi wachuuzi kuwajibika kwa usafi ili mazingira yawe salama.
Pichani
juu na chini ni wafanyabiashara wa Soko la Temeke Stereo, wananchi na
wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa Wziara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni
rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke (hayupo pichani).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akikambidhi Mkuu wa
Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto) vifaa vya kufanyia usafi
katika Soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70
ya Umoja wa Mataifa. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akivaa 'gloves' tayari
kushiriki zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya
Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Celestine Mushy wakifanya usafi katika maeneo ya wafanyabiashara
katika soko la Temeke Stereo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akibeba taka katika
soko la Temeke Stereo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Wilaya ya Temeke,
Sophia Mjema wakishiriki zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo
ikiwa ni sehemu ya kusheherekea maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa
Mataifa.
Wafanyakazi
wa Umoja wa Mataifa wakijumuika na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia
Mjema pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro
Rodriguez wakiendelea na zoezi la usafi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP),
Titus Osundina (kulia), Beatrice Mkiramweni pamoja na Jacqueline Namfua
wakifanya usafi kwenye maeneo ya soko la Temeke Stereo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP),
Titus Osundina akishiriki zoezi la kuzoa taka katika soko la Temeke
Stereo.
Umoja
ni Nguvu: Wafanyabiashara wa soko la Temeke Stereo, wafanyakazi wa
Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje wakishirikiana kwa pamoja
kufanya usafi katika soko hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
70 ya Umoja wa Mataifa.
Petra Karamagi na Nasser Ngenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa wakishikishiriki zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo.
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano alipomulikwa na kamera
Zoezi likiendelea.
Zoe Glorious katika ubora wake.
Usia Nkhoma Ledama akiwajibika katika zoezi la usafi soko la Temeke Stereo.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wafanyabiashara wakishirikiana katika zoezi hilo.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu (kulia) akiteta jambo na na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walioshiriki kwenye zoezi la kufanya
usafi wa mazingira katika soko la Temeke
Post a Comment