HERITAGE BROTHERS KUIMBA KWENYE MAKAMBI YA MAGOMENI MWEMBE CHAI MWAKA HUU
Msimu wa mikutano ya makambi imewadia tena mwaka huu kama zilivyotaratibu za Kanisa la Waadventista Wa Sabato Dunia,nchini Tanzania mikutano hiyo ambayo hutokea mara moja kwa kila mwaka itaanza mwezi julai katika makanisa mbalimbali.
Miongoni mwa mambo yanayovuta hisia za waumini wa kanisa hilo ni masuala ya uimbaji ambapo kumekuwa na utaratibu wa kuwa na waimbaji wageni wanaotoka kwenye maeneo tofauti na kanisa mahalia.
Miongoni mwa waimbaji wataohudhuria kwenye makambi ya Magomeni Mwembechai julai 19 hadi 25 mwaka huu ni waimbaji toka Lusaka, Zambia waitwao Heritage Brother ama HeriBros (Pichani)hili ni kundi lililoanzishwa mwaka 1986 linaloundwa na waimbaji wa kiume ambao huimba nyimbo za Acappella japo kwa uchache na zile zinazotumia ala za muziki.
Heritage Brothers wamewahi kuimba katika nchi za Sweden,Uingereza,Afrika Kusini,Botswana na Zimbabwe ambapo pia huwa wakiarikwa kuimba kwenye sherehe za kitaifa za balozi za Marekani,Uingereza,Kenya,Malawi nchini Zambia.
Waimbaji wa Heritage Brothers kwa sasa ni Alwyn Njoloma (1st Tenor) ,Blessed Chisenga (2nd Tenor) Abel Lyumbula (Baritone),Chimuka Musokotwane (Baritone) na Paddy Mukando (Bass).
Waliowahi kuimba kwenye kundi hili ambalo lina tuzo ya kundi la kiume la nyimbo za Injili ya CHAPRO mwaka 2014 Joshua Ziela,Alex Mwesa,Brian Lupiya,Bruce Mukuwa,Kenneth Lupiya[Marehemu ] na Ricky Chali
Post a Comment