MKUTANO MKUU WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO 2015 WAENDELEA SAN ANTONIO
Baadhi ya Viongozi wa Union 35 zilizopitishwa jana |
Mkutano Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani umeingia
katika siku ya pili hii leo ambapo
maelfu ya waumini wameendelea kuhudhuria mkutano huo unaofanyika San Antonio
Texas huko Marekani.
Mkutano huo ambao ni wa 60 toka kuanzishwa kwa mikutano mikuu
ya kanisa hilo ulimwenguni umeanza rasmi hapo jana kwa mapokezi maalumu wa
Unioni mpya 35 kutoka sehemu mbalimbali duniani ambapo Unioni ya kusini
mwa Tanzania,Union ya kaskazini mwa Tanzania na Unioni nne za Divisheni ya
Africa Mashariki na Kati ni miongoni mwa union hizo zilizopokelewa.
Katika siku ya kwanza ya mkutano huo umehitimishwa kwa
kuchagua kamati ya uchaguzi yenye wajumbe zaidi ya 250 huku Tanzania
ikiwakilishwa na Mwenyekiti wa Union ya Kusini mwa Tanzania Magulilo Mwakalonge
na Mwenykiti wa Union ya Kaskazin mwa Tanzania Mch Godwin Lekundayo na mshiriki
mmoja ambapo mapema hii leo kamati hiyo ilianza kazi yake.
Mkutano mkuu wa kanisa la Wadventista Wa Sabato Ulimwenguni
umeanza rasmi hapo jana na unatarajiwa kuhitimishwa Julai 11 mwaka huu kauli
mbiu ya mkutano huo ni Inuka uangaze Yesu anakuja.
Post a Comment