ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE NCHINI INDIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India kwa sherehe za ukaribisho wake rasmi nchini India kwa ajili ya ziara yake ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika asubuhi ya Juni 19, 2015.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu wa IndiaMheshimiwa Narendra Modi, na Rais Wa IndiaMheshimiwa Pranad Mukherjee wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Rais kikwete kuwasili katika ikulu ya India kwa mapokezi rasmi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Majeshi ya India liliandaliwa kwa ajili ya kumkaribisha kwa ziara rasmi ya Kiserikali nchini India katika sherehe za ukaribisho zilizofanyika asubuhi ya Juni 19, 2015.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa India wenye viwanda ambao wamewekeza nchini Tanzania muda mfupi baada ya kukutana nao Juni 18,2015
Picha na habari:http://blog.ikulu.go.tz/
Post a Comment