ZAMBIA YAWA MIONGONI MWA NCHI ZENYE WAUMINI WENGI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO DUNIANI
Rais wa Zambia Edger Lungu alijumuika hivi karibuni na maelfu ya Waadventista Wa Sabato katika uwanja wa michezo wa Heroes jijini Lusaka kusherekea kwa kanisa hilo kufikisha waumini milioni moja toka kuanzishwa kwake nchini humo ambako kuna idadi ya watu milioni 15.5
Zambia inaelezwa kuwa ndio nchi iliyo na waumini wengi wa kanisa la Waadventista Wa Sabato barani Afrika ambapo sasa inakuwa katika orodha ya nchi tatu duniani kuwa na waumini zaidi ya milioni moja wa kanisa hilo duniani, nchi zingine na idadi kwenye mabano ni Brazil (milioni 1.5), India (milioni 1.5) na Marekani (milioni 1.2).
Nchi zingine zenye idadi kubwa ya waumini ni Ufilipino iliyofikisha idadi ya waumini 918,669 Disemba mwaka jana,Kenya (824,185) na Zimbabwe (803,521) .
Kanisa hilo lina idadi ya waumini milioni 18.5 duniani kote mpaka sasa .
Post a Comment