MTANGAZAJI

BALOZI LIBERATA MULAMULA ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMTAIFA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Balozi Liberata Rutageruka Mulamula (Pichani) kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sasa Balozi Mulamula ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico.

Rais Kikwete pia amemteua Balozi Hassan Simba Yahya kuwa naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kwa sasa Balozi Yahya ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizarani hapo.

Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2015

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.