MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:WAIMBAJI WA TAMASHA LA NCHI SABA KUIMBA KWENYE MORNING STAR TV BIG DAY MAGOMENI MWEMBECHAI MACHI 14,MWAKA HUU

The Living Voices Choir  toka Uganda

Thee Family toka Zimbabwe
The Heirs Kutoka Dodoma
Agape Singers toka Musoma
The LightBearers Singers


Tamasha la Uimbaji ambalo limepewa jina la Festival of Love and Hope Home Coming Africa litakalofanyika Machi 15 mwaka huu  katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na IFM jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha waimbaji toka nchi 7 za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini .

Ratiba ya Machi 14 iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha hilo Warren Bright inaonesha kuwa siku hiyo ambayo pia itakuwa ni Morning Star TV Big Day itayofanyika katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai kanisa  waimbaji wote wa Home Coming Africa hasa wale wa nje ya jiji la Dar na nje ya nchi watakuwa katika program za Morning Star TV Big Day tukio ambalo litarushwa moja kwa moja toka kanisani hapo siku hiyo.


Siku hiyo ambapo kutakuwa na ibada moja waimbaji wa  The Living Voices Choir (Uganda),Fishers of Men (Zambia), Pillars of Faith (Kenya), Home Land Brothers (Uganda), na The Heirs (Tanzania) watahudumu kuanzia asubuhi, Vikundi na waimbaji wengine wote watahudumu mchana kwenye uimbaji.
 
Kumbuka tiketi kwa ajili ya tamasha hilo la Machi 15, 2015 zinapatikana kupitia kwa  Mpesa 0764 43 44 45 au Tigo pesa 0713 43 44 45

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.