MSHINDI WA TATU WA BSS 2007 LEAH MOUDDY AMSHUKURU MUNGU KUMRUDISHA KANISANI
Leah Mouddy (kulia) akiwa na Mtangazaji Maduhu |
Baadhi ya maoni na maswali yaliyoulizwa kwenye kipindi. |
Mshindi wa tatu wa Bongo Star Search (BSS) mwaka 2007 Leah Mouddy amesema anamshukuru Mungu kwa kumrudisha tena kanisani na hatimaye kufanikiwa kutoa album yake ya kwanza ya nyimbo za injili yenye nyimbo 8 iliyorekodiwa na Vocappella Media Production ya jijini Dar es salaam.
Leah anayetoka katika familia ya watoto sita ambao wote ni waimbaji wa nyimbo za injili akizungumza katika mahojiano maalum hii leo kwenye kipindi cha Lulu za Injili cha Morning Star Radio ambacho huongozwa na kutangazwa na Mtangazaji Maduhu amesema anamshukuru Mungu kwa kumpatia nafasi ya pili kurudi katika imani ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato.
Album ya kwanza ya mwimbaji huyo inataraji kutoka mwezi ujao,huku akifanya maandalizi ya kutengeneza video.
Post a Comment