KIGALI:SANTURI MWONEKANO NAMBARI 11 YA AMBASSADORS OF CHRIST KUTOKA APRIL MWAKA HUU
Baadhi ya Picha toka katika Video ya Toleo nambari 11 |
"Safari inaendelea mapambano yaendelea Siku za Kilio zimepita" ni maneno ya ujumbe mzito uliobebwa na toleo nambari 11 la Santuri Mwonekano ya Waimbaji mahili wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Remera yaani Ambassadors of Christ ambayo inatarajiwa kutoka mwanzoni mwa Aprili 2015,toleo hilo pia ni maandalizi ya toleo namba 12 la waimbaji hao toka Rwanda.
Makamu Mwenyekiti na Mkuu wa Mawasiliano wa Kwaya hiyo Ndugu Joseph Mutabasi ambaye huimba sauti ya nne amekaririwa hivi karibuni na blog hii akieleza kuwa toleo hilo nambari 11 litakuwa na nyimbo 10.
Baadhi ya nyimbo hizo ambazo zilitambulishwa rasmi katika kipindi cha Lulu za Injili cha Morning Star Radio nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi januari mwaka huu ni Rangi unazungumzia kuhusu Sabato,Kesheni Kaombeni ambao wameurejea kuuimba ukiwa ni wimbo wao uliopokwenye matoleo yao ya kati ya mwaka 1995 hadi 1998,Nimekupata Yesu na wimbo unaoebeba toleo hilo Siku za Kilio Zimepita
Post a Comment