JUBA:DR TED WILSON AFUNGUA MAJENGO MAWILI YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO HUKO JUBA SUDANI YA KUSINI
Nyumba ya Kulala Wageni ya ECD iliyofunguliwa |
Ofisini za Field za Kanisa la Waadventista Wa Sabato zilizoko Juba |
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Dr Ted Wilson akiwa katika ziara yake ya kutembelea nchi zilizoko katika Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati amezindua na kufungua majengo mawili huko Juba,Sudani ya Kusini ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika eneo hilo.
Akiwa Juba Ted Wilson amezindua na kuweka wakfu majengo mawili moja likiwa ni Ofisini za Field na Union ya Ikweta na jengo la pili ni la nyumba ya kulala wageni ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato la Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati(ECD).
Post a Comment