JUBA:KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO DUNIANI TED WILSON AWASILI JUBA,SUDANI YA KUSINI
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Dr Ted Wilson amewasili Juba,Sudan ya Kusini akitokea nchini Tanzania baada ya kushiriki kwenye sherehe za utume wa kanisa hilo(Mission Extravaganza) zilizofanyika kwa juma zima toka februari mosi mwaka huu na kuhitimishwa kwenye uwanja wa Taifa kuanzia Februari 4 hadi 7,mwaka huu.
Ted akiwa nchini Tanzania aliongoza ibada ya siku ya Sabato ambapo alihutubia waumini wa kanisa hilo wapatao 50,000 wanaounda Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati yenye nchi 11,huku ukihudhuriwa na Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal ambaye alizindua mkutano huo akiwataka waumini hao kuombea taifa la Tanzania kudumisha amani,upendo na mshikamano.
Mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na viongozi wandamizi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato toka yalipo makao makuu yake huko Washngton DC,Marekani ulishuhudia Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe akiufunga kwa kulipongeza na kulitaka kanisa hilo kutojiingiza katika migogoro ya aina yoyote.
Ted Wilson akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati aliwasili Juba na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo nchini humo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kutembelea nchini hiyo toka ilipojitenga na Sudani julai 9,2011.
Post a Comment