MTANGAZAJI

MORNING STAR TV SASA WAANZA KURUSHA NYIMBO ZA WAIMBAJI WALIZOZIREKODI

The PearlGate Singers walipokuwa wakirekodiwa
Mwenge SDA Choir walipokuwa wakirekodiwa
Angelos Singers
 
Ubungo Hill SDA Choir walipokuwa wakirekodiwa na Morning Star TV
Ushindi SDA Choir
Baada ya kufanya matengenezo ya studio zake mbili za kurekodia vipindi mbalimbali na kuanza kurekodi video za nyimbo za baadhi ya  waimbaji wa nyimbo za Injili katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania hatimaye Morning Star Televisheni imeanza kurusha nyimbo hizo hewani katika matangazo yake ya majaribio yaliyoanza Julai 7,mwaka huu kupitia kisimbuzi cha TING na Digitek.

Blog hii ambayo imekuwa ikifuatilia kwa karibu baadhi ya waimbaji wa Kwaya na Vikundi ambao wamekuwa wakirekodiwa na kituo hicho kupitia studio zake za kisasa zilizopo katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Ushindi, juzi na jana imeshuhudia nyimbo zilizorekodiwa juma lililopita zikionekana kupitia Morning Star TV,baadhi ya nyimbo hizo ni za Angelos Singers,Mwenge SDA Choir na The Pearlgate Singers zikiwa katika ubora.

Kumekuwa na matatizo mbalimbali ya kimaadili na ufundi kutokana na ubora hafifu kwenye baadhi ya video za kwaya mbalimbali na vikundi vya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini zilizorekodiwa kabla ya kuanza kwa Morning Star TV jambo ambalo linaleta changamoto kwa kituo hicho katika uchaguzi wa nyimbo za kurusha kwenye matangazo yake ya majaribio yanayoendelea.

1 comment

Unknown said...

Jamani Natafuta Wimbo Wa Watoto Wa The Voice Pf Unaitwa Hakuna Mkamilifu Asanten Kwa Kuwa Utanitekelezea Kazi Yangu Mawasiliano Ni Dannymyson21@gmail.Com

Mtazamo News . Powered by Blogger.