|
Makamu wa Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Mch Geofrey Gabriel Mbwana akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kanisa hilo Kanda ya Mashariki mwa Tanzania Mch Mark Walwa Malekana |
|
Mch Geofrey Gabriel Mbwana akihutubia |
|
Mch Mark Walwa Malekana akisalimu waumini |
|
Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Lugalo |
|
Waimbaji wa Mwananyamala SDA Choir |
|
Waimbaji wa Mbezi Beach SDA Choir |
|
Waimbaji wa Kwaya ya KKKT Usharika wa
Salasala wakifuatilia |
|
Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la RC la Mbezi Beach |
Makamu wa
mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Mchungaji Geofrey
Gabriel Mbwana amewataka waumini wa madhehebu mbalimbali nchini kudumisha mahusiano mema japokuwa wanamitazamo tofauti katika masuala ya imani.
Akihutubia
hii leo kwenye sabato maalum ya ujirani mwema na uimbaji iliyofanyika kwenye kanisa la Waadventista Wa
Sabato Mbezi Beach jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na waumini wa madhehebu
mbalimbali Mchungaji Mbwana amesema kuna haja ya waumini hao kuyatazama zaidi
masuala ya imani wanayofana na kuyajadili kwa upendo na amani yale
wanayotofautiana.
Naye
Mwenyekiti wa Konferensi ya Mashariki mwa Tanzania (ETC) ya Kanisa la
Waadventista Wa Sabato Mchungaji Mark Walwa Malekana akimshukuru Kiongozi huyo
kwa ukubali wake kushiriki kwenye ibada hiyo amesema pamoja na watanzania
kutoka katika madhehebu mbalimbali hapa nchini basi wanapaswa kutokuwa na chuki
kutokana na tofauti za kiimani.
Ibada hiyo
ambayo ilirushwa moja kwa moja na Morning Star Radio katika kipindi cha Ibada
makanisani pia ilihudhuriwa na Waimbaji wa Kwaya ya KKKT Usharika wa
Salasala,Kwaya ya Kanisa la RC la Mbezi Beach na Kwaya za Makanisa
ya Waadventista Wa Sabato Lugalo,Mbezi Beach na Mwananyamala.
Post a Comment