MARA:MAKAMPUNI YACHANGIA UJENZI WA MABWENI YA SHULE YA NYASINCHA YALIYOUNGUA MWEZI SEPTEMBA
Mgodi
wa dhahabu wa African Barrick Gold North Mara kwa ushirikiano na kampuni saba
wametoa msaada wa zaidi ya shilingi 23 milioni kusaidia ujenzi wa vyumba vitatu vya
mabweni ya wavulana katika Shule ya Sekondari
Nyansincha vilivyoungua moto Septemba 15 mwaka huu.
Katika
msaada huo mgodi huo umetoa shilingi 13 milioni, kampuni ya Mara kaskazini bati 30, duka la vifaa vya ujenzi Chakechake
mifuko 20 ya saruji yenye thamani ya shilingi 800,000, kampuni ya AKO vitanda 26 vya deka, Kundi la Kemambo shilingi 200,000,
Gimunta Champion shilingi milioni moja, Borrtech (T) ltd shilingi 3 milioni na kampuni ya
Magnet ilitoa shilingi 1.5 milioni.
Akikabidhi
msaada huo kwa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wa Sabato Meneja wa mgodi wa ABG North Mara, Garry Chapman amesema, kupatikana
kwa msaada huo kutoka kwa wadau ni umoja na ushirikiano walionao katika kazi
huku wakionyesha kuguswa na tukio la mabweni matatu kuteketea na kuwafanya wanafunzi kupata
shida ya masomo.
Akipokea
msaada huo Mkuu wa shule hiyo Japhet Mugini alisema msaada
huo utawasaidia kufikia katika hatua nzuri ambayo itawafanya wanafunzi waanze
kulala katika vitanda vyao wenyewe tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wanalala
wawili wawili kenye kitanda kimoja.
Mabweni
matatu ya wavulana ya Shule ya Sekondari ya Nyansicha
yalichomwa moto septemba 15 majira ya saa 11 jioni na mwanafunzi wa kidato cha pili Michael Kimunye aliyedhaniwa
kuwa na ugonjwa wa mapepo ambapo moto huo uliteketeza mali ya
wanafunzi na shule yenye thamani ya sh, 113.6 milioni.
Post a Comment