KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO AWATAKA WATU KUMWEKA MUNGU MBELE
Mwenyekiti
wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato
katika Konferensi ya Mara Mchungaji Daudi Makoye amewataka watu
kuyashika maneno ya Mungu ili waweze kufanikiwa katika maisha yao.
Kiongozi
huyo ametoa agizo hilo mwishoni mwa juma jijini Mwanza wakati akihutubia kwenye
kilele cha mkutano wa Mkutano wa Chama cha Wanataaluma na wajasiriamali
Waadventista Wa Sabato
Tanzania (ATAPE) uliokuwa
ukifanyika kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini humo ambao pia uliwahusisha watu
wenye ulemavu wa ngozi albino.
Katika
mkutano huo ambapo kulifanyika
ibada ya kuwaombea watu
wenye ulemavu wa ngozi albino na
taifa la Tanzania Mchungaji Makoye amesema jamii inatakiwa kuonyesha juhudi ya
kumweka Mungu mbele ili awe ngao na kinga katika maisha.
Amesema
mtu yeyote asitegemee akili ya mtu mwingine ili aweze kufanikiwa bali kila
mmoja afanye kwa uwezo na akili yake mwenyewe binafsi aliyopewa na Mungu na
siyo kutegemea utajiri kutoka kwa viungo vya albino.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa ibada hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arusha Dr Moses Muneja amewataka watu wote kuwa
na moyo wa huruma na kujitolea kutoa misaada yao inapohitajika bila kujali
kupata malipo.
Mkutano
huo ambao ulikuwa wa kwanza kuwahusisha watu wa rika na kada mbalimbali ulihudhuriwa na Mwakilishi wa Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Sheikh Abdalah Hija na Mwenyekiti wa Kanisa la
Waadventista Wa Sabato wa Unioni ya Kaskazini Mwa Tanzania Dr Godwin Lekundayo.
Post a Comment