VIONGOZI WA KANISA WAOMBA WAUMINI KUSHIRIKI KATIKA SIKU YA AMANI DUNIANI-SEPTEMBA 21,MWAKA HUU
-->

Viongozi wa Kanisa la Waadventista wa
Sabato Duniani wamewataka waumini wa Kanisa hilo kuungana na kushiriki katika
siku ya amani itakayoadhimishwa na umoja wa Mataifa Septemba 21 mwaka huu kwa kufanya maombi ya mchana katika muda wa dakika moja ya ukimya iliyopangwa kwa siku hiyo.
Wito huo umetolewa kufuatia taarifa ya
maandalizi iliyotolewa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon inayowataka
watu kuakisi amani na kuongeza kuwa ni lazima kila mtu kupingana na sababu
zozote zinazoweza kuleta mapigano na kuelezea kuwa amani ndiyo njia watu wote
wanayopaswa kusafiri kwayo hatua kwa hatua.
Taarifa iliyotolewa na Kanisa la Waadventista wa Sabato
kupitia kwa mkurugenzi wa idara ya uhusiano na uhuru wa dini John Graz imesema waumini wa Kanisa hilo
wanapaswa kuwa na amani na watu
wote,na kuweka bayana kuwa Yesu Kristo mwenyewe anawataka wafuasi wake kuwa
watu wa amani ndani ya jamii na kuwa mkono wa mbaraka kwa watu wengine.
Graz amesema ili kuboresha amani
Duniani Kanisa linapaswa kuwekeza katika maendeleo ya Elimu,Afya,haki na uhuru
kwa watu wote ndiyo maana kama kanisa hilo lina Shule,Hospital na taasisi
mbalimbali za kusaidia raia.
Chanzo:ANN
Post a Comment