DAR ES SALAAM:WASHIRIKI WA KANISA WATAKIWA KUTOISHI MIJINI BILA KAZI
Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Unioni
Misheni ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji James Machage amewataka washiriki wa kanisa hilo wanaoishi mijini bila
kufanya kazi kurudi vijijini na kujihusisha na kazi za kilimo ili kuleta
maendeleo ya kanisa na jamii kwa ujumla.
Mchungaji Machage ametoa agizo hilo katika kanisa la
Waadventista Wa Sabato Magomeni
anapoendesha mkutano wa juma la uamusho la uwakili lililoanza sabato iliyopita
ambapo amesema inashangaza watu wengi kuishi katika maeneo ya miji mikubwa kama
Dar es salaam na hawana kazi za kufanya hali inayofanya waongeze msongamano wa
watu wakati kuna maeneo makubwa vijijini
yanayohitaji kuendelezwa.
Machage amesema kuwa serikali haina uwezo wa kuwapatia watu
wote ajira hivyo inapaswa wananchi watumie elimu waliyonayo kukabiliana na
mazingira na kujipatia maendeleo yao wenyewe huku akisisitiza kuwa miji yenye
msongamano wa watu kama Dar es salaam waishi watu walio na kazi tayari.
Mchungaji Machage ambaye kitaaluma ni mtaalamu wa masuala ya
anga amesema imefika wakati sasa kwa waumini wa kanisa kuweka juhudi katika
kutumia elimu waliyonayo kufanyakazi kwa bidii na kujipatia maendeleo binasfi
na kusaidia miradi mbalimbali ya kanisa na kama mtu anaelimu na hana kazi ya
kufanya ni vema kuchukua maamuzi ya kwenda kijijini kulima na si kuishi mjini
wakati hana jambo la kufanya.
Post a Comment