PWANI:MWONGOZO WA VIWANGO VYA WADAU WA HABARI NA UJUMBE SAHIHI KUHUSU UKIMWI (VVU) WATOLEWA
Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP) hivi
karibuni umezindua mwongozo wa Taifa wa
Kupitia na Kuhakiki nyenzo za habari, elimu na mawasiliano ya kubadili tabia
kwa lengo la kuboresha habari na mawasiliano yanayofanywa na Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii na wadau
wake kwa lengo la kuthibiti kuenea kwavirusi vya UKIMWI (VVU).
NACP iliyopo
chini ya Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii ikiwa na jukumu la kusimamia masuala
yakinga, tiba, matunzo na misaada kwenye nyanja ya UKIMWI ka tika
sekta ya afya nchini, imezindua mwongozo huo kwa wadau wa habari, elimu na
mawasiliano (IEC) na mawasiliano ya Kubadili Tabia (BCC), mjini Bagamoyo.
Mwongozo huo wa kwanza kwenye sekta ya afya unalenga
kuweka viwango vya kitaifa kwa wadau wa mawasiliano ambapo nyenzo zote za
machapisho na za kielektroniki za IEC/BCC zitapaswa kuhakikiwa na idara hiyo
kwa lengo la kuboresha ujumbe unaotolewa.
Lengo kubwa la mwongozo huo huo ni kuhakikisha
matangazo yote yanayohusu kinga, tiba, matunzo na misaada kwenye nyanja ya UKIMWI
yana hakikiwa ubora ili kutoa ujumbe sahihi kwa walengwa katika jitihada za
serikali za kuunga mkono jitihada za wadau wanaojihusisha na afua za ugonjwa
huo.
Katika dibaji ya mwongozo huo, Mganga Mkuu wa
Serikali, Dk Donan Mmbando anasema licha ya juhudi kubwa ya uenezaji na
upatikanaji wa shughuli za habari na mawasiliano kuhusu VVU na UKIMWI
nchini,bado kuna baadhi ya ujumbe usiostahili unaotolewa kwa walengwa.
Post a Comment