MTANGAZAJI

KINACHOELEZWA KUWA NI BARUA YA RAIS WA BRAZIL KWENDA KWA NEYMAR


 Mwandishi wa habari wa BBC  Natalie Pirks katika wasifu wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter Julai 5,2014 ameweka barua hii akiielezea kuwa ni barua ya Rais wa Brazil kwa Mchezaji wa Timu ya taifa ya nchi hiyo Neymar aliyeumia wakati wa mchezo wa soka wa Kombe la Dunia kati ya timu yake na timu ya Colombia ambapo Juan Carlos Zuniga alimgonga nyota huyo kwa nyuma na kuumia .

Mfupa wa Neymar unaoshikana na uti wa mgongo ulivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia.

Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.

Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.