DAR ES SALAAM:BOT KUTOA KUZINDUA SARAFU YA SHILINGI 500
Benki
kuu ya Tanzania (BOT),inatarajia kuzindua sarafu ya shilingi 500 itakayochukua
nafasi ya shilling mia tano ya noti.
Akizungumza
hapo jana katika banda la BOT kwenye viwanja vya maonesho ya kimataifa ya
biashara ya 38 ya sabasaba jijini Der es salaam,afisa mwandamizi wa benk
hiyo,Hawa Muro,amesema kuwa wamefikia hatua hiyo kutokana na kuwapo kwa
utunzaji mbovu wa noti ya shilingi 500.
Muro
amesema kuwa katika uchunguzi uliofanywa wamegundua kuwa wananchi wengi
wanashindwa kuitunza noti hiyo kutokana na mzunguko mrefu iliyonayo kwa
watumiaji.
Amesema
BOT,inaamani kuwa sarafu ya shilingi 500 ndiyo itakayo dumu kwa muda mrefu
katika mzunguko wa pesa nchini.
Muro
amesema mchakato wa mabadiliko hayo
ambao unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha mwaka wa 2014/2015 ambapo
sarafu hiyo itazinduliwa na benki hiyo ili wananchi waanze kuitumia.
Post a Comment