SOKO LA KARUME (MCHIKICHINI) LATEKETEA KWA MOTO
Soko la Mitumba la Karume baada ya kuungua kwa moto (Picha kwa Hisani ya Dar es salaam Yetu Blog) |
Soko la Mitumba la Karume (Maarufu Mchikichini) lililoko katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam,limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.
Wakizungumza na waandishi wa habari hii leo baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo wamesema kuwa mali zote zikiwemo ngu,viatu,mabegi na bidhaa nyingine zimeteketea kwa moto na kwa sasa hawaelewi cha kufanya.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa inawezekana moto huo ni hujuma kutokana na mgogoro wa muda mrefu baina yao na halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Wamesema mgogoro huo umesababishwa na uamuzi wa halmashauri hiyo kutaka kuwaondoa kwa madai yakulifanyia ukarabati soko hili bila kuwapatia eneo lingine.
Hata hivyo Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Slaa amewataka wafanyabiashara hao kujiepusha kuwa watabiri na kwamba halmashauri inafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.
Post a Comment