WAZIRI MKUU AITAKA WIZARA KUTATUA TATIZO LA MADAWATI TANZANIA
Waziri Mkuu
wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda amesema shule za msingi nchini humo
zinakaribiwa na upungufu wa madawati takribani milioni moja na nusu na akaitaka
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipe kipaumbele suala la kupunguza tatizo
hilo.
Waziri Mkuu
ametoa agizo hilo mwishoni mwa juma lililopita wakati akihutubia mamia ya
wakazi wa mkoa wa Dodoma ambao walihudhuria uzinduzi wa wiki ya Elimu Tanzania
kwenye uwanja wa Jamhuri .
Waziri Pinda
alisema takwimu zinaonesha kuwa Tanzania inahitaji madawati 3,302,678 wakati
madawati yaliyopo ni 1,837,783 kwa hiyo kuna upungufu wa madawati 1,464,895
katika shule za msingi.
Kutokana na
mahitaji hayo Waziri Mkuu anasema kuwa endapo serikali itaamua kutengeneza
madawati 100,000 kwa mwaka kwa gharama ya shilingi bilioni 12 itachukua miaka
15 kumaliza tatizo hilo ili kuziba pengo lililopo sasa.
Anasema ni
lazima hatua madhubuti zichukuliwe na serikali kumaliza tatizo hilo kwani
inatia aibu na hakuna sababu ya kuendelea kuona wanafunzi wakisoma huku wamekaa
chini.
Post a Comment