ALBINO WAITAKA SERIKALI YA TANZANIA KUTUNGA SERA MAALUM YA MATIBABU YA KANSA YA NGOZI
Chama cha
Albino Tanzania kimeita serikali ya Tanzania kutunga sera maalum ya kupambana
na ugonjwa wa saratani ya ngozi,kwani mkakati uliopo sasa unaubaguzi kwa watu
wenye ualbino.
Chama hicho
kimetoa tamko hilo kupitia risala yake iliyosomwa na Mwakilishi wa Chama cha
Albino Tanzania, Hussein Kibindo kwenye maadhimisho ya siku ya watu wenye
ualbino iliyofanyika jana jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa
saratani ya ngozi ni changamoto inayoongoza kwa kusababisha vifo kwa watu wa
kundi hilo,hali inayosababisha watu wenye ualbino kuishi nusu umri tofauti na
watu wengine.
Akizungumza
kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kwenye maadhimisho hayo
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr
Seifu Rashid amesema kuwa serikali itaendelea kufanya jitihada za kukabiliana
na changamoto zinazolikabili kundi hilo ili kuhakikisha linapata haki ambazo
linazozidai.
Post a Comment