WATU 15 WAHOFIWA KULIWA NA MAMBA HUKO KIGOMA,TANZANIA
Zaidi ya watu 15 wakazi wa kijiji cha
Chagu,kata ya Mtego wa Noti,Wilaya ya uvinza wanahofiwa kufa kwa kuliwa na
mamba katika Bwawa la Mngonya liloko kilomo mkoani Kigoma.
Matukio hayo yameathiri shughuli za
kijamii ,zikiwemo shughuli za uvuvi na kupunguza nguvu kazi ya kijiji hicho
katika kata ya Mtego,hali iliyosababisha wanakijiji hao kutokuwa na imani na
watendaji na viongozi wa idara husika kutokana na kufumbia macho tatizo hilo.
Katika hali isiyo ya kawaida baadhi wa
wakazi wa kijiji hicho wamewaambia wanahabari kuwa , kufuatia ukimya huo wa muda mrefu wa
watendaji na viongozi hali hiyo imewalazimu kufikisha kilio chao kwa mwenyekiti
wa CCM mkoani Kigoma Daktari Walid Amani Kabouro.
Bwawa la Mngonya liloko Kilomo ni nguzo
ya maendeleo kwa wananchi wa kijiji cha Chagu katika kufanikisha shughuli za kijamii zikiwemo shughuli za uvuvi
lakini inavyooneka wananchi hao wamekua wakiathiriwa na mamba walioko kwenye
Bwawa hilo.
Post a Comment