MAAMBUKIZI YA VVU KWA WATOTO MKOANI LINDI BADO NI TISHIO
Zaidi ya watoto 31 kati ya watoto 820
waliozaliwa mkoani Lindi kati ya kipindi cha mwaka 2013/2014 wamebainika kuwa na maambukizi
ya virusi vya ukimwi kutoka kwa wazazi wao.
Hayo yameelezwa na Mganga mkuu wa Mkoa
wa Lindi Daktari Yusuph Sonda katika uzinduzi wa huduma ya matumizi ya dawa Za
kupunguza makali ya virusi vya ukimwi (VVU) kwa wajawazito.
Daktari Sonda ameongeza kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na shirika la Egpaf kupitia mradi wa
kudhibiti ukimwi wameanzisha mpango mkakati wa kupunguza maambukizi ya ukimwi
kutoka kwa mama kwende kwa mtoto toka asilimia 20 hadi asilimia tano.
Pamoja na juhudi zinazofanywa na wadau
kuhakikisha huduma hizo zinapatikana,Mkoa wa Lindi bado unakabiliwa na changamoto
mbalimbli zikiwemo za upungufu wa vituo vya kutolea huduma hizo hadi
kufikia sasa kuna vituo 98 tu vinavyotoa huduma lakini hitaji la mkoa ni vituo
210.
Post a Comment