WANANCHI MKOANI SHINYANGA WAITAKA SERIKALI KUTUMIA RASILIMALI ZA MADINI KUBORESHA SHULE
Wananchi Mkoani Shinyanga wameitaka
serikali kutumia rasilimali za madini zilizopo kuboresha mazingira ya shule za
msingi na sekondari kama nyumba za walimu vifaa vya kufundishia ili kupata
walimu bora na wataalamu wenye ujuzi.
Wakizungumza na waandishi wa Habari kwa nyakati
tofauti baadhi ya wananchi hao,wamesema kuwa serikali inapaswa kufanya
tathimini ya mafanikio yaliyopatikana kupitia migodi ya madini ya
Buzwagi,Bulyanhulu na Mwadui katika kuchangia maendeleo ya jamii.
Licha ya serikali kujivunia mafanikio
yaliyopatikana tangu uhuru kwa kuongeza sekondari kata,lakini shule hizo
zinakabiliwa na matatatizo mengi.miongoni mwa matatizo hayo ni uhaba wa nyumba
za walimu pamoja na maktaba za kisasa.
Mkoa wa shinyanga kupitia zao la madini
linachangia zaidi ya asilimia kubwa katika pato la taifa lakini hali
ambayo haijasaidia kutoa ufumbuzi wa
changamoto ya elimu mkoani humo.
Post a Comment