HALMASHAURI YA TEMEKE NA MKAKATI WA USAFI WA MAZINGIRA
Jumla ya watuhumiwa 172
walikamatwa na wengine 92 kupewa onyo
kali na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam katika oparesheni ya usafi wa mazingira iliyoanza
mwezi machi mwaka huu ili kuondoa kero za uchafuzi wa mazingira kwa makusudi
katika halmashauri hiyo .
Taarifa ya Afisa Afya wa
Manispaa ya Temeke,William Muhemu aliyoitoa hivi karibuni kwa vyombo vya habari
katika oparesheni hiyo watuhumiwa 80 walitozwa faini za papo kwa papo na
kupatikana jumla ya shilingi 4,120,000
na wengine 45 walifikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea.
Katika operation hiyo jumla ya
mabanda 415 na meza 2193 zilivunjwa na ombaomba 74 walikamatwa na kurudishwa
makwao huku zoezi hilo lenye lengo la usafi wa mazingira,uzalishaji na utupaji
ovyo wa taka ngumu na utumiaji wa vyoo likihusisha jumla ya nyumba 3614 na
majengo ya biashara 225 yaliyokaguliwa.
Taarifa hiyo inaonesha kuwa kuwa
ujenzi holela wa makazi, vyoo,ukosefu wa miundombinu kwenye makazi yasiyo rasmi
na uhaba wa mabwawa ya maji machafu ni miongoni mwa mambo yanayochangia
uchafuzi wa mazingira katika eneo la halmashauri hiyo .
Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke ina ukubwa wa kilometa za mraba 656. Ina jumla ya watu 1,368,881 kwa taarifa
ya sensa ya mwaka 2012.na tarafa 3 za Mbagala, Chang’ombe na Kigamboni. Pia ina
kata 30 na mitaa 180.
Post a Comment