WAKAZI WA UKEREWE MWANZA WAIOMBA SERIKALI KUDHIBITI WIZI WA MADAWA YA BINADAMU
Wakazi wa wilaya ya ukerewe mkoani
Mwanza wameiomba serikali kudhibiti vitendo vya wizi wa madawa pamoja na vifaa
tiba vinavyofanywa na baadhi na watumishi wa sekta ya afya ili kuwaondolea
wananchi kero ya kuzitafuta huduma hizo katika maduka ya watu binafsi ambapo
hakuna udhibiti wa bei.
Wakazi hao wametoa ombi hilo wakati
wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi CCM
mkoani Mwanza ambapo pia wametaka kukomeshwa wavuvi haramu vilivyo shamiri katika Ziwa
Victoria.
Upatikanaji usioridhisha wa dawa
katika baadhi ya zahanati na vituo vya afya mkoani Mwanza umeendelea kuwa kikwazo
katika mapambano dhidi adui maradhi ambapo baadhi ya wakazi wa kijiji cha
Nduruma Wilayani Ukerewe wamehoji sababu ya zahanati ya kukosa dawa na kutakiwa
kwenda kununua dawa kwenye maduka yanayomilikiwa na watumishi wa zahanati hiyo.
Hali hiyo imebainika wakati wa ziara
ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi
CCM mkoa wa Mwanza inayolenga kusikiliza kero za wananchi.
Kijiji cha Bukanda wananchi
wamewasilisha maombi kutaka kukomeshwa kwa uvuvi wa kutumia zana haramu
ulioshamiri katika ziwa Victoria.
Post a Comment