MTANGAZAJI

UTAFITI:UVUNJAJI WA HAKI YA KUISHI WAENDELEA KUSHAMILI NCHINI TANZANIA

Takwimu za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania zinaonesha kuwa vitendo vya uvunjaji wa haki ya kuishi vimeendelea kushamili miongoni mwa wanajamii nchini Tanzania katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Akitoa ufafanuzi wa ripoti ya haki za Binadamu nchini Tanzania ya  mwaka 2013 kwa waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salam,Mkurugenzi wa utetezi na Maboresho wa kituo hicho Wakili Halord Sungusia amefafanua kuwa mwaka 2012 watu 1234 waliuawa huku watu 1669 walipoteza maisha kwa mwaka 2013 kwa kuuawa na wetu wenye hasira kali.

Takwimu hizo zinamaanisha kuwa kila siku watu 4 wanapoteza maisha yao kutokana na mauaji hayo ambapo jiji la Dar es salaam ndilo ambalo liliongoza kwa kuwa na idaidi ya watu 240 waliouawa katika wilaya za Kinondoni,Ilala,Temeke na mkoa wa Mwanza ukiwa katika nasafi ya pili ambako watu 195 waliuawa.

Utafiti wa ripoti hiyo umebaini kuwa mauaji mengi ya aina hiyo yanatokea hasa katika maeneo ya mijini na watu wa jinsi ya kiume ndio wanaoonekana kuhusishwa zaidi huku eneo la Kaskazini Pemba likionesha idadi ya mtu mmoja tu aliyepoteza maisha.

Kwa upande wa imani za kishirikina inaonekana wanaume 505 na wanawake 260 walipoteza maisha na maeneo ambayo bado yanaongoza kwa tatizo hilo ni Geita,Shinyanga,Mwanza na Simiyu.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.