MTANGAZAJI

WAKAZI WA KIJIJI CHA GIBASO,TARIME WAMLALAMIKIA MWEKEZAJI



Wakazi wa kijiji cha Gibaso kilichoko kata ya Nyarokoba Wilayani  Tarime  wamesema kuwa wanaitaji utaratibu ufuatwe dhidi ya mwekezaji wanayedai kuwa amepora  ardhi yao yenye zaidi ya hekari 2000 .

Uamuzi huo umefikiwa jana katika mkutano wa mkuu wa hadhara wa kijiji hicho uliowahusisha wana kijiji zaidi ya 300 chini ya Mwenyekiti wa Kijiji,Robert Morenda na Diwani wa Kata ya Nyarokoba Mustafa Masiani  ambapo walidai kuwa  kuchukuliwa kwa eneo hilo ni kuwataka wawe wakimbizi kwenye nchi yao hali ambayo itawafanya watahabike kimaisha kwa vile wana zaidi ya miaka 50 wakilima na kuishi eneo hilo.

Wamelitaja eneo hilo kuwa ni katika kitongoji cha Byantang'ana
linalopakana  na kijiji cha Mrito kuwa limetaifishwa kwa kupewa mwekezaji Isack and sons co. ltd . huku wakisema kuwa mwekezaji huyo anadai  kuwa anataka kuliendeleze eneo hilo kwa kulima zao la alizeti jambo ambalo si kweli.

Wamedai  kuwa wanachokiona wao eneo hilo kuna  machimbo ya dhahabu ya Byantang'ana nakuwa ndicho kinachomvuta mwekezaji huyo.

Mwandishi  wa habari hizi  alishuhudia shughuli za kusafisha eneo hilo zikiendelea huku wananchi wanaomiliki eneo hilo wakitakiwa  kuondoka na mazao yao kukatwa na mkonge uking’olewa na kampuni hiyo..

Uchunguzi umebaini kuwa mgogoro huo uko katika mahakama ya wilaya ya Tarime  toka mwezi wa kwanza mwaka huu, na inaonekana kuwa  wizara ya ardhi nyumba na makazi imetuma barua kwa wanakijiji hao ikionesha  imemtuma mpimaji  Isack Marwa aliyetakiwa afike mwezi wa nne mwaka huu katika kijiji hicho kupima eneo hilo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.