MTANGAZAJI

TAZARA YASIMAMISHA HUDUMA ZAKE



Uongozi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), umesimamisha huduma ya usafiri wa treni ya mizigo na abiria  kutoka Dar es Salaam hadi Tunduma.

Hatua hiyo imefuatia mgomo wa wafanyakazi wa TAZARA kudai  mshahara wa kuanzia Februari hadi Aprili, mwaka huu.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (Trawu) kuitisha mgomo kuanzia Mei 12, mwaka huu kwa wafanyakazi wote kususia kuingia kazini hadi mshahara wao utakapolipwa.

Mkuu wa Kitengo cha Habari Tazara, Conrad Simuchile, amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijiji Dar es Salaam jana.

Amesema katika Mikoa ya Tanzania vituo vyote vya kati ya Dar es Salaam na Tunduma na baadhi katika Mkoa wa  Zambia stesheni ya Kasama hawafanyi kazi.

Simuchile amesema kuwa uamuzi wa  kuondoka kazini bila kufuata taratibu,unasababisha usumbufu kwa abiria,wateja na Shirika kupata hasara,hivyo hawawezi kulipa mshahara wa Mei wakati wafanyakazi wamegoma.

Amesema shughuli za kawaida zitaendelea kati ya Nakonde na New Kapiri - Mposhi upande wa Zambia, ambayo inahusisha treni ya abiria Mei 13, mwaka huu kutoka New Kapiri – Mposhi  na kuishia Nakonde. na kudai kuwa uongozi wa Tazara unafanya jitihada zote ili kuhakikisha usafiri wa treni unarejea .


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.