MTANGAZAJI

TANZANIA ZANZIBAR INADAIWA SHILINGI BILIONI 294



Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, jana alitangaza bajeti ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2014/15 na kusema serikali mpaka kufikia mwezi wa Machi 2014, inadaiwa Sh. bilioni 294 sawa na ongezeko la asilimia 17

Amesema deni hilo limeongezeka ikilinganishwa na deni la Sh. bilioni 252 lililokuwapo Machi 2013.

Amesema ukuaji huo umetokana na kutolewa fedha kwa ajili ya miradi inayoendelea kama vile ya ujenzi wa njia ya ndege kuruka na maegesho ya ndege, miradi ya maji safi na salama na miradi ya barabara.

 Kati ya deni hilo, karibu Shilingi  bilioni 212 deni la nje linalomaanisha ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa na Shilingi karibu bilioni 204 kwa Machi 2013.

Asilimia 88 ya deni la nje imedhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na asilimia 12 Serikali ya Zanzibar na kuwa hadi Machi 2014, deni la ndani nalo liliongezeka hadi Shilingi bilioni 83

Amesema hali hiyo imetokana na kuongezeka kwa mikopo kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), deni la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) na deni la wastaafu. Mwaka 2014/15 serikali inatarajia kukusanya Shilingi bilioni 707  kulinganisha na Shilingi  bilioni 658  za mwaka 2013/14.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.