VIJANA WADOGO WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO NJIRO ARUSHA KUTOA MAFUNZO KWA JAMII
Kanisa la waadventista wasabato mtaa
wa Njiro jijini Arusha,kupitia idara ya vijana wadogo wa chama cha wavumbuzi na watafuta njia
imeandaa mpango maalumu wa kuifanya jamii ya wakristo kurudi katika misingi ya
maadili bora.
Mpango huu ambao
utahusisha waadventista na wasiowaadventista wasabato mkoani Arusha
unatarajiwa kuwakutanisha vijana zaidi ya mia tatu na hamsini katika kanisa la
Lemara ambapo watapatiwa mafunzo mbalimbali yanayohusu imani ya kweli pia namna
ya kuwapelekea wengine Injili iokoayo.
Akizungumza na mwandishi wa habari Mchungaji wa mtaa wa Njiro, Nuhu suleiman amesema kuwa Tukio hilo
litakalofanyika may 17 2014 litawafanya vijana kujua na kutambua ni wapi
misingi ya kijana mwenye maadili ilipo na ni kwa jinsi gani kuiendea. katika
siku hiyo Vitabu zaidi ya mia mbili vya tumaini kuu vitasambazwa kwa watu
mbalimbali katika maeneo ya lemara.
Kwa upande wake Youze
Mangashi Kiongozi wa Idara hiyo ya vijana Mtaa wa njiro amesema Rali hiyo
inalenga kuwaandaa na kuwahamasiha vijana kwa ajili ya kambi kubwa
conference ya kaskazini mashariki mwa Tanzania litakalofanyika Kwakoa mwezi wa
sita mwaka huu.
Post a Comment