MTANGAZAJI

MAMA AMSAMEHE MUUAJI WA MWANAE WA PEKEE, NA SASA WANAISHI NYUMBA MOJA

 
Oshea akiwa amekumbatiana na mama wa marehemu
Kwa hali ya kibinadamu ni vigumu kuamini ama kukubali kumsamehe mtu aliyekutendea unyama wa ajabu ama jambo lililoondoa furaha yako lakini pia kwa msaada wa Mungu jambo hili ni jepesi sana hasa kama Kristo anatawala maisha yako. Mama mmoja aitwaye Mary Johnson's mkazi wa Minnepolis nchini Marekani amemsamehe muuaji wa mwanae wa pekee na kumkaribisha kupanga nyumba moja.

Muuaji huyo aliyefahamika kwa jina la Oshea Israel alimuua Laramiun Byrd mwaka 1993 wakiwa katika sherehe ambako kulitokea mkwaruzano wa kutoelewana na kijana huyo akijikuta akimuua mwenzake,
ambapo mama mzazi wa marehemu alishinikiza sheria kali ichukuliwe dhidi ya muuaji wa mwanae ambaye kwa wakati huo alikuwa na miaka 16 alimuita kuwa ni mnyama na anahitaji kifungo. Oshea alihukumiwa miaka 25 na nusu jela pamoja na kutumikia jamii mara amalizapo kifungo chake.

Lakini miaka michache baadae mama huyo alianza kumtembelea kijana huyo gerezani mara kwa mara  na kujua namna msamaha unavyofanya kazi na kukaririwa katika maongezi yake kwamba kutosamehe ni sawa na ugonjwa wa kansa ambao utakutafuna ndani na nje hivyo ameamua kusamehe.
 
Mama huyo ambaye huimba mda wote afanyapo shughuli zake alimtambulisha kijana huyo kwa mwenye nyumba yake mara baada ya kutoka jela mwaka 2010, ambapo mwenye nyumba alikubali kumpangisha na sasa wanaishi nyumba moja kama majirani na kushiriki kanisani pamoja, huku kijana huyo ambaye kwasasa anamiaka 37 amekuwa akifanya kazi za kijamii kama kuomba msamaha na kuonyesha fadhila kwa mama huyo. Lakini pia mama huyo kwasasa ameanzisha kampuni iitwayo 'From Death to Life'  yenye lengo la kuhamasisha msamaha kati ya watu wahalifu na familia zilizoguswa na watu hao. Hivi karibuni GK iliripoti habari ya familia moja nchini Iran iliyoamua kumsamehe muuaji wa mtoto wao wa pekee, ambapo bila hivyo ilikuwa muuaji huyo anyongwe hadharani mbele yao.
 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.