SEKTA YA HABARI NA ELIMU ZAOMBWA KUKABILI CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA NCHINI TANZANIA
Sekta ya habari
na elimu zimeelezwa kuwa ni nguzo imara
ya kunusuru mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi hapa nchini.
Hayo
yamebainishwa na mtafiti wa mabadiliko ya hali ya hewa Dr Radisilaus Chang’a
kutoka mamlaka ya hali ya hewa Tanzania
TMA wakati akizungumza na wadau
katika semina ya kujadili changamoto ya mazingira kutoka wilaya ya
Iringa vijijini.
Semina hiyo
imelenga kuwaelemisha waandishi wa habari pamoja na walimu namna
watakavyoielimisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira ili kuendana na mabadiliko
ya hali ya hewa hususani mkoa wa iringa
Radisilaus
amewataka walimu wa shule za secondari mkoani Iringa kufikisha elimu ya
mazingira kwa wanafunzi wao ambao wanaweza kuisambaza elimu hiyo katika
jamii inayowazunguka.
Pia ameiomba
jamii kufuata maelekezo wanayoyapata kutoka kwa watalaam juu ya shughuli zao
wanazozifanya hususani kilimo na matumizi ya nishati ya mkaa na kuni kwani
kauli mbiu ya mapambano hayo ni kata mti
panda miti
Post a Comment