MTANGAZAJI

MKOA WA GEITA HAUNA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI

Mkoa wa Geita nchini Tanzania  wenye wilaya tano hauna Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa muda mrefu sasa.

Ofisa Mtendaji wa Mahakama mkoani Geita  Lothan Simkoko amekaririwa na vyombo vya habari akieleza kuwa serikali mkoani Geita ina mpango wa kujenga mahakama ya hakimu mkazi ili kuwapunguzia wananchi adha ya kufuatilia mbali huduma ya utatikanaji wa haki kwa wakati.

Geita ni miongoni mwa mikoa mipya nchini Tanzania iliyoanzishwa hivi karibuni ambako wakazi wake hupata  huduma za  maamuzi ya ngazi  za mahakama ya mkoa huipata mwanza na kusababisha usumbufu kwa wananchi wa mkoa huo.

Wilaya tano za mk0a wa Geita ni
Nyang’wale,Geita,Bukombe Chato,pamoja na Mbogwe ambazo zote kwa pamoja hupeleka malalamiko ya kesi zake mkoani humo.` 


Mahakama hiyo inayotarajiwa kuanza muda si mrefu itaanza kwa kutumia jengo la mahakama ya mwanzo ya Nyankumbu jengo ambalo ni mali ya mahakama ,ambapo mahakama ya mwanzo itahamia kwenye nyumba za Nyanza.

Ofisa mtendaji huyo amewaomba mahakimu mkoani humo kuendelea kusikiliza kesi kwa muda mfupi ili kuepuka malalamiko yanayojitokeza kwa wananchi, na kutoa ushauri kesi wa zisizokuwa na msingi kuachana nazo ili kuepuka mrundikano wa mahabusu gerezani.


Simkoko amewaomba wananchi mkoani humo kushirikiana kushirikiana kwa karibu ili kubaini mtumishi wa mahakama ambaye atajihusisha na rushwa kutoa taarifa ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria .

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.