MAFURIKO YASABABISHA MAWASILIANO YA BARABARA KATI YA IFAKARA,MRIMBA MALINYI NA MAHENGE MOROGORO KUKATIKA
Mvua
zinazoendelea kunyesha hapa nchini zimesababisha mafuriko katika mji wa ifakara
mkoani Morogoro na kuharibu miundo mbinu ya barabara,madaraja na kivuko cha
ifakara kwenda Mrimba mkoani humo.
Akizungumza
na Morning Star Radio mmoja wa abiria waliokwama kwa siku nne kutokana na
kukosa usafiri wa kuelekea Mrimba kutoka
mji mdogo wa Mwembetogwa Ifakara,Mei
Ibogo anasema sehemu kubwa ya barabara inayoelekea Mrimba imejaa maji na
barabara hiyo haipitiki kwa sasa.
Anasema ameshuhudia sehemu kubwa ya barabara kuelekea
kivuko cha Mto Kilombero kinachovusha abiria kwenda Malinyi
kutoka Ifakara imechukuliwa na maji na hivyo abiria wanaoelekea mrimba na mahenge
kukosa usafari kutokana na uharibifu huo.
Mei amesema
yeye pamoja na abiria wengine wameshauriwa kusubiri maji ya pungue ama watumie
usafari wa mitumbwi japo kwa wale wanaofahamu kuogelea kwakuwa maeneo mitumbwi
hiyo inapita kumekuwa na changamoto ya kuzidiwa na maji na kupelekwa katika
mwelekeo mwingine.
Naye mkazi wa
Mwembetogwa Khamisi Mumbira pamoja na kueleza kuwa mafuriko ya mwaka huu kuwa
makubwa kuyashuhudia amesema usafiri ambao waweza kutumika sasa kutoka ifakara
kwenda Mrimba ni treni ama trekta japo ameitupia lawama serikali kwa
kutoshughurikia miundo mbinu ya barabara katika eneo hilo
Post a Comment